Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein
amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali katika taasisi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa
na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar,DKT
.Abulhamid Yahya Mzee, DKT Shein amemteuwa Ali Salim Mchenga kuwa Afisa
Tawala Mkoa wa Kusini,Unguja.DKT Makame Ali Ussi kuwa Afisa Tawala Mkoa
Kaskazini Unguja na Khamis Salim Mohd Shambi kuwa Afisa Tawala Mkoa
Kaskazini Pemba.
Aidha DKT Shein amewateuwa
Mohamed Abdulla Ahmed kuwa Afisa Tawala wa Wilaya Mjini,Unguja.Omar
Abdulla Juma kuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Kati, Unguja na Juma Abdulla
Hamad kuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Katika Ofisi ya Rais Fedha
,Uchumi na Mipango ya Maendeleo DKT Shein amewateuwa Abdi Khamis Faki
kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar,Hafidh Ussi Haji kuwa Naibu
Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar.Seif Shaaban Seif kuwa Kamishna
wa Mitaji ya Umma. Mwita Mgeni Mwita kuwa Kamishna wa Bajeti.DKT Rahma
Salim Mahfoudh kuwa Kamishna wa Ukuzaji Uchumi katika Tume ya Mipango ya
Zanzibar na Bihindi Nassor Khatib kuwa Kamishna wa Fedha za Nje.
Wengine aliewateuwa katika
Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano ni Capt Abdulla Juma Abdulla kuwa
Mkurugenzi wa Shirika la Bandari na Abdi Omar Maalim ambae ameteuliwa
kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini.
Halkadhalika Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein Amewateuwa
wafuatao kutoka Wizara ya Biashara ,Viwanda na Masoko ambapoMwanahija
Almas Ali kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC. Suleiman Juma Jongo Naibu
Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC. Abdulmalik M .Bakari kuwa Ofisa
Mdhamini wa ZSTC, Pemba na Khatibu Mwadini Makame kuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Viwango la Zanzibar(Zanzibar Bureau of Standards)





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)