Beki
wa timu ya Yanga, Oscar Joshua (kulia) akimtoka mshambuliaji wa African
Lyon, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, jana jioni. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na
ushindi wa Mabao 4-0. Bao la kwanza la Yanga, limefungwa na kipa wa
African Lyon, Juma Abdul, aliyejifunga katika dakika 8, kipindi cha
kwanza, bao la pili limefungwa na Haruna Niyonzima kwa mkwaju wa penati,
dakika ya 54, baada ya beki wa Lyon Semi Kessy, kumchezea rafu, Msuva
katika eneo la hatari. Goli la tatu limefungwa na Simon Msuva, katika
dakika ya 72, kufuatia pasi safi ya Frank Dumayo na bao la nne
limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 90+2, baada ya pasi safi ya
Idrisa Rashid.
Mchezaji wa timu ya Yanga Khamis
Kiiza akiwania mpira mbele ya golikipa wa timu ya Africa Lyon Juma Abdul
mwenye namba 30 mgongoni wakati wa mchezo wao wa kirafiki kwenye uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kocha wa timu ya Africa Lyon
Muargentina Pablo akionekana kulalamikia jambo kwenye benchi la ufundi
la timu yake wakati timu yake ilipokutana na timu ya Yanga katika
mchezo wa kirafiki kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Kikosi cha timu ya Africa Lyon kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano huo kuanza.
Kikosi cha timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Taifa kabla ya kuingia uwanjani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)