Viamwana wa bendi ya African Stars
Twanga Pepeta wakionyesha umahiri wao wa kunengua katika onyesho lao
la sikukuu ya Eid El Fitri liliofanyika ndani ya Mango Garden
Kinondoni jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo huku mashabiki wa
bendi hiyo wakijumuka kwa pamoja katika kusherehekea sikukuu hiyo
inayosherehekewa na waislamu kote duniani, Burudani ilikuwa ni kali na
ya kufurahisha mkutokana na uwezo mkubwa wa wanamuziki wa bendi hiyo
huku wakipewa sapoti na mashabiki wao waliokuwa wamefurika ukumbini
hapo, Mpiganaji wa Fullshangweblog.com Bw. Philemon Solomon alikuwepo
ukumbini hapo ili kushuhudia yaliyojiri na hizi ndiyo Taswira
alizotuletea kutoka ukumbini hapo endelea kupata burudani mdau
Mwimbaji na Kiongozi wa bendi hiyo
Luiza Mbutu wa pili kutoka kulia akiimba pamoja na waimbaji wa bendi
hiyo wa bendi hiyo wakati ilipokuwa ikitumbuiza katika onyesho lake la
Sikukuu ya Eid El Fitri kwenye ukumbi wa Mango Garden Kinondoni usiku wa
kuamkia leo.
Wanenguaji wa kiume wa bendi hiyo
wakishirikiana na mwanamuziki Luiza Mbutu wakionyesha jinsi ya kupinda
mgongo katika onyesho hilo.
Mmoja wa wanengaaji matata wa bendi hiyo akiwaonyesha mashabiki jinsi ya kusugua kisigino.
Mashabiki wa bendi hiyo
wakijimwaga stejini wakati bendi hiyo ikifanya vitu vyake kwenye ukumbi
wa Mango Garden usiku wa kuamkia leo
Mastaili ya bendi hiyo yakionyesha mbele ya mashabiki wa muziki
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)