Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwasili kwenye Uwanja wa Kwa Mbombe katika kijiji cha Madizini, Kata ya Mtibwa mkoani Morogoro ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Opereshi Sangara juzi.
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini
kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema amefungua matawi
katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi August 18,2012.
Katika
ziara hiyo, Lema aliambatana na Mbunge wa Arumeru Masariki Mh Joshua Nassari(wa pili kulia)
pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM kabla ya kujiengua na kujiunga na
Chadema mapema mwezi Aprili mwaka huu, Ndg James Ole Millya, ambao nao kwa
nyakati tofauti walipata fursa ya kuzunumza.
Mbali
na suala la uzinduzi na upokeaji wanachama wapya, Lema alifanya harambee ya
kukusanya fedha kusaidia shughuli za chama hicho katika Kata hiyo ambapo jumla
ya Sh 219,500 zilichangwa na wananchi.
Akiondoka
eneo hilo, Lema alilazimika kuwatuliza mamia ya watu waliokuwa wanafuatilia
msafara wake ili kuepusha kutokea mwanya kwa watu wenye nia mbaya kuleta vurugu
na uharibifu wa mali. Baadae msafara wake ulikatiza mitaa ya Stand Kuu ya mabasi makubwa
na kisha kuelekea bustani ya City Park huku njiani akishangiliwa sana na baadhi
ya watu wakinyoosha vidole kama ishara
ya ushindi.
Wanachama wapya aliojiunga na chadema wakigombania kadi za chama hicho
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini
kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema akiunguruma kwenye uzindusi wa matawi
katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi August 18,2012.
Jitihada za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za kuwafikia wanachi
ili kunadi sera zake, hususan katika mikutano inayoendelea katika mkoa
wa Morogoro, zilikumbana na vikwazo mbali mbali katika baadhi ya maeneo,
kama inavyoonyesha pichani, mtaro uliochimbwa katika barabara ya
kuingia kijiji cha Namgezi kitongoji cha Kambi ya Keya jimbo la Ulanga Mashariki, kwa lengo la kuzuia magari yasipite.Picha na Joseph Senga
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)