Na Mwandishi Wetu
WANANCHI na wahanga wa bomoabomoa kwa wakzi wa nyumba za kota za eneo la Gerezani, Kariakoo, Dar es Salaam, wametahadharishwa kuacha kuchukua hatua yoyote kutokana na suala lao kuwa mahakamani.
Wahanga hao wanasubiri kujua kama watafidiwa kitu chochote kutokana
na bomoabomoa iliyowakumba hivi karibuni, na kupata fidia ya uharibifu
na uvunjifu wa haki za wakazi hao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakili Sengondo Mvungi,
anayelisimamia suala hilo, alisema wakazi hao wanatakiwa kuwa watulivu
kwa sasa wakati suala lao likishughulikiwa kisheria, huku akiwaahidi
kulisimamia ipasavyo.
Mvungi, ambaye anatoka katika ofisi ya mawakili ya South Law
Chambers, alisema suala lao litashughulikiwa bila kuwa na tatizo lolote
likisimamiwa na yeye, na kuwasihi wanachi na wakazi wa eneo hilo kuwa na
subira.
Alisema: "Suala la haki ya umiliki tajwa na fidia itokanayo na
utwaaji wa eneo hilo na Serikali na fiudia ya uharibifu na uvunjifu wa
haki za binadamu za wakazi wa Gerezani ziko mahakamani kwa mujibu wa
kesi namba 44 ya mwaka 2012."
Mvungi, alisema taarifa zilizotajwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Usafiri wa Haraka (DART) kwa wahanga wakapokee fidia zao linakiuka amri
ya Mahakama Kuu, iliyotajwa Juni 28, 2012, na kuwashauri kutotii agizo
hilo.
Aidha, wakili huyo anayewasimamia wananchi wa Gerezani, amewataka
kuhudhuria katika kikao cha pamoja na wakili wao (Mvungi),
kitakachofanyika Agosti 11 mwaka huu (Jumamosi) katika ukumbi
watakaoarifiwa na kamati.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)