Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Mtendaji
mkuu wa Mahakama pamoja na Msajili mkuu wa Mahakama na msajili wa mahakama ya
rufani katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Walioapishwa
leo ni Mtendaji mkuu wa Mahakama Bwana Hussein Katanga,Msajili Mkuu wa Mahakama
Bwana Ignus Paul Kitusi na Msajili wa Mahakama ya Rufani Bwana Panterine
Muliisa Kente.Pichani Mtendaji mkuu wa Mahakama Bwana Hussein Katanga akila
kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo
asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya
pamoja na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) pamoja na maofa
waandamizi wa mahakama aliowaapisha leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.(Wapili
kushoto) ni Mtendaji mkuu wa Mahakama
Bwana Hussein Katanga,(Wanne kushoto) ni Msajili Mkuu wa Mahakama Bwana
Ignus Paul Kitusi na kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Bwana Panterine
Muliisa Kente.Picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)