Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongazana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar
(PBZ) Juma Amour, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam jana Agosti 8, 2012 kuhudhuria hafla ya futari
iliyoandaliwa na Benki hiyo na kufutari pamoja na baadhi ya Waumini wa
dini ya Kiislamu walioalikwa.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad
Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali
‘kujisevia’ futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya
Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu pamoja na Makamu wa Rais
Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika
hafla hiyo, jana Agosti 8, 2012.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza
baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati
wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa
Zanzibar (PBZ) na kufuturu pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na
baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo,
jana Agosti 8, 2012.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour,
akizungumza machache kuhusu kazi na utendaji wa kazi za Benki hiyo ya
Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na malengo yake wakati wa hafla hiyo
ya futari iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi
ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari
iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakipata
futari wakati wa hafla hiyo.
Baadhi
ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari
iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakishiriki
kuomba dua ya pamoja wakati wa hafla hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi
wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana Agosti 8, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman
Kova, na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya
futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa
Zanzibar (PBZ) jana, Agosti 8, 2012 katika ukumbi wa Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh, Abdulla Tarib Abdulla na
baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari
iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana katika
ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin
Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)