TASWIRA ZA MABOMU YA MACHOZI YALIVYORINDIMA MTAA WA KONGO KARIAKOO JANA MARA BAADA YA VURUGU KUZUKA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TASWIRA ZA MABOMU YA MACHOZI YALIVYORINDIMA MTAA WA KONGO KARIAKOO JANA MARA BAADA YA VURUGU KUZUKA

Mmoja wa majeruhi wa mabomu ya machozi kwenye vurugu hizo akiondolewa eneo la soko la Kariakoo baada ya kuanguka chini kutokana na milipuko hiyo, ambayo iliambatana na mawe yalikuwa yakirushwa na vijana waliokua wakitetea upande mmoja wa ugomvi huo.
Askari wa Kikosi Cha kutuliza Ghasia FFU wakiweka ulinzi mkali eneo la Kariakoo baada ya kufunga mtaa wa Kongo na ya jirani kutokana na kuibuka vurugu zilizotokana na ugomvi wa nyumba ambayo kwa maelezo ya watu wa karibu nyumba hiyo ilikuwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka 20 kati ya wamiliki na wapangaji kutokana na kutengeneza hati feki.
Mitaa ya Kituo cha Polisi Msimbazi Kariakoo ikiwa mitupu bila ya watu wengi kama ilivyozoeleka ni askari tu ndio waliokuwa wakiranda kwenye eneo hilo.
Mtu ambaye alijitambulisha kuwa ndie mwenye nyumba hiyo ambayo inamilikiwa na mama yake, ambapo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wameipigania haki yao kwa miaka ishirini hadi leo wanaipata kutokana na kesi waliyofungua mahakamani wakidai kunyang'anywa nyumba yao na wapangaji kwa kutengeneza hati feki.
Nyumba inayo gombaniwa na kuzua tafrani kabla haijaanza kuvunjwa eneo la mtaa wa Kongo Kariakoo.
Hapa vijana wa kazi wa kampuni ya Yono Auction Mart iliyopewa tenda ya kusimamia ubomoaji wa nyumba hiyo chini ya ulinzi mkali wa pilisi wakiendelea na kazi kwenye nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Kongo
Mashuhuda nao walikuwepo tangu zoezi linaanza na walikuwepo pia wanaoufahamu mgogoro huo na kudai kuwa nyumba hiyo anadhulumiwa mzaramo na Mwarabu kwasababu anapesa, lakini wengine wakasema nyumba hiyo imeuzwa mara tatu tofauti na kuzua mgogoro huo.
 Mtaa wa Kongo ukiwa hauna mweupe
 Mtaa wa Mchikichini Kariakoo ukiwa hauna watu kutokana na vurugu zilizotokea jana
 Mtaa wa Mkunguni ambao huwa na pilikapilika nyingi ukiwa mtupu kufuatia wafanyabiashara kufunga biashara zao

 Askari Polisi wakimdhibiti mmoja wa vijana waliokamatwa katika vurugu zilizotokea katika mtaa wa Kongo na Mchikichi jijini Dar es Salaam jana kufuatia mgogoro wa kugombea nyumba namba 86 inayomilikiwa na Samiri Said
 Askari Polisi akiweka mabomu ya machozi katika bunduki yake huku akiangalia hali ya usalama wake.
 Askari Polisi akijiandaa kurusha mabomu ya machozi ili kukabiliana na vijana waliokuwa wakirusha mawe.Picha Zote na Francis Dande wa HABARI MSETO BLOG
 
 
DAR ES SALAM, Tanzania

RISASI na mabomu ya kutoa machozi jana vilirindima katika maeneo ya Kariakoo baada ya mtu mmoja kuvamia nyumba kwa zaidi ya miaka 40 akidai kuwa ni yake.

Hali hiyo imekuja baada mmiliki halali wa nyumba hiyo, Samiri Said kushinda kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo mahakama ili mtaka mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Shaban Hassan kuondoka katika nyumba hiyo.

Akizungumza katika eneo la tukio kiongozi wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Isaac Nguku alisema walifika eneo hilo kwa amri ya Mahakama kwa lengo la kukabidhi nyumba hiyo kwa Said.

Amesema kuwa hata hivyo, walipofika katika eneo hilo majira ya saa 5:00 asubuhi walikuta kundi la vijana ambao inasadikika kuwa waliandaliwa na Hassan kwa ajili ya kukwamisha zoezi hilo.

Nguku alisema baada ya kuona hali hiyo waliamua kuomba msaada kutoka polisi ambapo walifika na kuanza kuwatawanya vijana hao.

“Vijana hao hawakuridhika ndipo wakaanza kuturushia mawe kutoka kila kona walizokuwa wamejipanga kitendo hicho kilisababisha askari kufyatua risasi za moto juu huku wakipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya mbali” alisema Nguku.

Baada ya vijana hao kutawanyika mitaa minne inayozunguka nyumba hiyo ilifungwa, mitaa hiyo ni pamoja na Kongo, Mkunguni, Tandamti na Mchikichini

Naye mmiliki wa nyumba hiyo, Said alisema wavamizi hao walipanga katika nyumbani hiyo tangu mwaka 1972 ambapo baada ya hapo wakajitengezea hati bandia kwa lengo la kumdhulumu mama yake mzazi.

Alisema kitendo hicho kiliwafanya wafikishe kesi hiyo mahakamani ambako waliwakilisha hati zao ambazo zimewafanya washinde kesi hiyo, mvamizi huyo  kuamriwa aondoke kitendo alichokipinga huku akikata rufaa za mara kwa mara lakini hata hivyo akawa anashindwa mara zote.

Nyumba hiyo inayogombewa iko mtaa wa Karikoo kitalu namba 86, hata hivyo wakati zoezi hilo likiendelea mvamizi huyo alikuwa  ndani kwa ajili ya kutumikia kifungo cha siku 21.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages