BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika wiki baada ya mpambano wao mkali na mahasimu wao Sikinde uliofanyika Jijini Dar es salaam pamoja na Zanzibar baada ya kutoa burudani ya Iddi sasa wamerudi kwa ajiri ya kutoa burudani ambapo wamesema kuwa wataanza kutoa burudani siku ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosiwatakuwa Kilimani Pub Staki Shari, na jumapili watamariza wiki endi katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni
Akiongea
, Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua
kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea baada ya kusherekea sikukuu .
Alitaja vibao vinavyotamba kwa sasa vya bendi hiyo kuwa na Suluhu wa Sabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga mbali na nyimbo hizo bendi hiyo itapiga nyimbo zake zilizotamba zamani zikiwemo Asha Mwanasefu,Cheusi Mangara,mwana Mkiwa na nyingine nyingi zilizotamba kipindi hicho
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)