Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mselem Ali
Na Idara ya Habari,MAELEZO -Zanzibar
Taasisi mbalimbali za kidini hapa
nchini zilizopata usajili rasmi kwa Mrajis Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar zimekanusha kuhusika na tamko lililotolewa na Amiri Mkuu wa
Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mselem Ali la Waislamu wa Zanzibar wagomee
kushiriki katika Sensa ya Watu na Makaazi Kitaifa inayotarajiwa
kufanyika Jumapili ijayo.
Wakizungumza na Katibu wa Mufti
wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga Wawakilishi wa Taasisi hizo wamelaani
tabia ya Uamsho ya kujipa Mamlaka ya kuzisemea Taasisi hizo.
Aidha,wameitaka Jumuiya ya Uamsho
kuthibitisha ni kikao gani kilichokaa na kuzungumza na Taasisi za
Kidini na kuamua kwa pamoja kutowa tamko hilo la kupinga kushiriki kwa
Waislamu katika Sensa.
Aidha, wameihakikishia Afisi ya
Mufti na Serikali kuwa watashiriki katika Sensa ili kusaidia maendeleo
ya Zanzibar na kutatua baadhi ya migogoro ya kijamii na sio kujiingiza
katika siasa na kupingana na Serikali kama ambavyo imekuwa ikifanya
Jumuiya ya Uamsho.
Taasisi zimewataka Waislamu kushirikiana na Serikali na kuachana upotoshaji unaofanywa na Uamsho.
Aidha, wameitaka Jumuiya ya Uamsho
kuachana mara moja kutumia kivuli cha umoja wa Taasisi za kidini
Zanzibar wanapoamua mambo yao kwani Jumuiya hizo nyingi hazikubaliani na
Sera yao ya fujo na vurugu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)