Taarifa Kwa Umma Kutoka Benki Kuu Ya Tanzania - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taarifa Kwa Umma Kutoka Benki Kuu Ya Tanzania


Katika Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe 10 Agosti 2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye maana kuwa “Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu”. Katika habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo kufuatia ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa benki na utawala bora.

Benki Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama zilivyo benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufanya biashara na benki hii kama kawaida.

IMETOLEWA NA 
BENKI KUU YA TANZANIA
11AUGUST 2012

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages