HATIMAYE Shindano la Miss Utalii mwaka 2012
linaloshirikisha Wilaya mbili za Kinondoni na Ilala limepata mdhamini ambaye ni
Kampuni ya ‘Rash Sports and Entertainment’ (RSE).
Shindano hilo litafanyika Agosti 14 mwaka huu,
kwenye Ukumbi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam ambako litashirikisha
warembo 30 kutoka katika wilaya hizo mbili.
Akizungumza na Fullshangweblog jijini leo, wakati
akimnadi mfadhili huyo, Mkurugezi wa Shindano hilo, Methuselah Magese alisema
kujitokeza kwa mfadhili huyo, kutasaidia kuamsha ari ya washiriki kwa
kuutangaza vizuri mkoa wa Dar es Salaam kiutalii.
Alisema mfadhili huyo, ameahidi kusaidia kipindi cha
mazoezi kilichobaki cha wanyange hao, ambako awali mazoezi hayo yalikuwa
yakifanyika katika hoteli ya Traventine na hivi sasa kuhamia Lamada.
“Lengo la shindano hili ni kutaka kuligeuza jiji la
Dar es Salaam kuwa kivutio cha utalii kama ilivyo kwa mikoa ya Kilimanjaro na
Arusha”alisema Magese.
Akizungumzia maandalizi kuhusu warembo hao, Magese,
alisema warembo wote 30 wanafanya mazoezi kwa juhudi pia wako vizuri kiakili
katika kuchambua mada mbalimbali walizojiandalia kwa ajili ya siku fainali.
Naye Mkurugenzi wa RSE, Rashid Mrisho, alisema kwa
kuwa biashara nyingi zimekuwa zikiendelea kupitia matangazo, hivyo kuwasaidia
warembo hao ni moja ya fursa itakayoleta chachu katika kuvitangaza viashiria vyote vya utalii
vilivyoko katika jiji hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)