Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana
nyumbani kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 baada ya kumtembelea
na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John
Evans Atta Mills aliyezikwa jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani
kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 wakati alipomtembelea
kiongozi huyo mpya wa Ghana na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais
wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya
kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts Farms
Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti
11, 2012
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi
yanayolimwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la Bomarts
Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam nje kidogo ya
jiji la Accra leo Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa
shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa
Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya mananasi katika
shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra.
Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd. Bw Emmanuel B.
Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27.
Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya
1980 kujionea ukulima huo wa matunda.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)