MDAU
wa michezo na aliewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Villa Squad
Fc ya Magomeni jijini Dar es Salaam, Ally Kindoile amejitosa kuwania
nafasi ya Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA),
unaotarajiwa kufanyika mkoani humo Agosti 28 mwaka huu.
Kindoile
ambaye pia aliwahi kukaimu kwa muda nafasi Mwenyekiti wa Villa kabla ya
kushuka daraja, alisema kuwa, amechukua uamuzi wa kuwania nafasi hiyo,
ili kuinua soka la Mkoa wa Kilimanjaro na pia kurudisha sifa na heshima
iliyokuwepo miaka ya nyuma kwenye mchezo huo.
Kindoile,
alibainisha mipango yake mikubwa kuwa ni pamoja na kupandisha timu ligi
kuu na kunyakua mataji mbalimbali ikiwamo Taifa Cup.
“Naomba
wadau wa michezo mkoani hapa, kwa pamoja kushirikiana kwa hali na nguvu
ili kuleta maendeleo ya soka, kwa kuwa pamoja tukishirikiana tunayo
nafasi ya kurudisha hali na morali kwa vijana na wanamichezo ndani ya
Kilimanjaro na siku za usoni tupate timu yetu itakayoshiriki ligi kuu
Tanzania Bara,” alisema Kindoile.
Licha
ya kuwa mdau wa michezo, aliwahi kuchezea timu mbalimbali zikiwemo
Simba B na Idrisa Fc, kwa sasa ni mdau mkubwa wa timu ya Kilimanjaro
Rangers ya mkoani Kilimanjaro na amekuwa kwenye mstari wa mbele katika
kusaidia vijana kwenye soka, huku kwa vipindi tofauti alifanikiwa
kuipandisha timu ya Villa Ligi Kuu kwa vipindi viwili ikiwemo msimu
2010-2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)