Spika Makinda akiuasa ujumbe huo
kuhudhuria mkutano huo kwa lengo la kuikwamua na kuivusha Tanzania
kutoka hatua moja kwenda nyingine.
Mhe. Ole Medeye akiutanbulisha ujumbe wa Tanzania utakaohudhuria
mkutano huo. Ujumbe huu unahusisha taasisi mbalimbali kama vile
Halmashauri, Sumatra, Wasafirishaji, wataalamu wa Ardhi na wataalamu wa
Makazi
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.
Anne Makinda akiwa ofisini kwake leo na mgeni wake, Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Goodluck Ole Medeye. Mhe Medeye
alikuja kumpa Mhe Spika muhtasari wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu
Makazi utakaofanyika Napole, Italia kuanzia tarehe 1 hadi 6 Septemba
2012 ambapo Spika makinda na maspika wengine kutoka bara la Afrika
wamealikwa kushiriki.Picha na Prosper Minja-BUNGE
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)