Mwandishi
wa Habari Mwandamizi Jenerali Ulimwengu akizungumza na wajumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba (hawapo pichani) wakati alipokutana nao leo
jumatatu tarehe 13. Agosti.2012 na kubadilishana nao mawazo na uzoefu.
Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Waziri Mkuu mstaafu
Joseph Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani
na Katibu wa Tume hiyo Assaa Rashid.
Mtaalamu
wa historia na mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar, Profesa
Abdul Sheriff (kushoto) akifafanua jambo katika mkutano wa na Wajumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam
(Jumatatu, Agosti 13, 2012). Wengine ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu
Joseph Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani
na Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid (kulia).(Picha na Tume ya Katiba)
Na Mwandishi Wetu
Wajumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameendelea kukutana na kubadilishana
mawazo na uzoefu na Wataalam mbalimbali kuhusu Katiba Mpya kwa lengo la
kuongeza uelewa wao na leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012), kwa nyakati
tofauti, Wajumbe wamekutana na Prof. Abdul Sheriff na Ndg. Jenerali
Ulimwengu.
Tayari
Tume hiyo imeshawaalika na kukutana na kwa nyakati tofauti na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mzalendo Jaji Mark Bomani, Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Pius Msekwa na
Mhadhiri wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa
Shivji.
Prof.
Sheriff ni mtaalam wa historia na mwanaharakati wa siku nyingi kutoka
Zanzibar na kwa muda mrefu amekuwa akishiriki na kutoa mada katika
makongamano mbalimbali yanayohusu Katiba. Ndg.Ulimwengu ni Mwanasheria
na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi ambaye pia ameshiriki na kutoa
mada katika makongamano mbalimbali yanayohusu Katiba Mpya.
Akizungumza
wakati akiwakaribisha, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji
Mstaafu Joseph Warioba alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatambua
kuwa Tanzania ina wataalam wanaoweza kutoa mchango mkubwa katika
mchakato wa mabadiliko ya Katiba na kuwasihi wanapopata nafasi wasisite
kuwasilisha maoni yao kwa Tume.
“Tukipata
nafasi, huwa tunawaomba wataalam kama ninyi kuja kubadilishana mawazo
na Wajumbe wa Tume. Ni matumaini yangu kuwa Wajumbe wa Tume watafaidika
sana na utaalam wako katika kupanua mawazo,” alisema Jaji Warioba katika
mkutano uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu
Mstaafu Agustino Ramadhani, Wajumbe wengine wa Tume na Sekretarieti ya
Tume.
Jaji
Warioba aliongeza kuwa Tume imejiwekea utaratibu wa kukutana na makundi
mengine mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kubadilishana mawazo na
kupokea maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Akiongea
katika mkutano huo leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012), Prof. Sheriff
pamoja na kushukuru kwa kualikwa na Tyume, alizungumzia uzoefu wake
katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba unaoendelea na kutoa maoni yake
katika masuala mbalimbali yakiwemo Muungano na Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba.
Kwa
upande wake, Ndg. Ulimwengu ambaye amekutana na Tume hiyo leo
(Jumatatu, Agosti 13, 2012) mchana, pamoja na mambo mengine,
alizungumzia umuhimu wa kuandika Katiba Mpya itakayotumiwa na Watanzania
kwa miaka mingi ijayo katika kuwaletea maendeleo ya kijamii, kiuchumi
na kisiasa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)