Washiriki
wa mashindano ya Mercedes Cup 2012 ya Boti zinazokwenda na Upepo
(Sailing Boat) wakiwa wamekusanyika Yatch Club jijini Dar kabla ya
kuanza mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors
yanayofanyika kila mwaka.
Pichani ni Boti zinazotumika katika mashindano hayo.
Washiriki wakianza mashindano hayo kuzunguka fukwe karibu na kisiwa cha Bongoyo.
Washiriki wakichuana.
Boti iliyombeba Refarii wa mashindano hayo pamoja na wasimamizi wengine.
Tuzo za washindi zikiwa mezani.
Meneja
Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed(katikati) akijadili jambo na
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) pamoja
Catamaran Representative wa Dar es Salaam Yatch Club Andrew Boyd.
Mkurugenzi
wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (katikati) akizungumza
machache baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo amewataka watu
kujitokeza kwa wingi kila mwaka na kutoa shukrani zake kwa wote
walioshiriki kufanikisha mashindano hayo. Kushoto ni Meneja Masoko wa
CFAO Motors Tharaia Ahmed na kulia ni Andrew Boyg wa Dar es Salaam Yatch
Club.
Washiriki na familia zao wakisubiri kuanza kwa zoezi la kutoa zawadi.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akimkabidhi zawadi Refarii wa mashindano hayo.
Mkurugenzi
wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akikabidhi zawadi kwa moja
ya timu iliyoshiriki mashindano hayo na kushika nafasi ya nne.
Washindi wa tatu David na Sarah Scott wakipokea zawadi na tuzo.
Katika picha ya kumbukumbu na wadhamini wa mashindano CFAO Motors.
Pichani Juu na Chini Washindi wa pili Paul na Kim Troll wakipokea zawadi kutoka CFAO Motors.
Meneja
Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akikabidhi Kombe kwa timu ya
washindi wa kwanza wa mashindano ya Boti zinazokwenda kwa kutumia upepo
(Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 Al Bush na Jeppe yaliyofanyika
katika fukwe za Yatch Club Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh. Mashindano hayo
yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akigawa Champagne kwa washindi.
Mshindi wa kwaza akifungua Champagne.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (Kulia) na Mkurugenzi wa
Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) katika picha ya pamoja
ya washindi wa kwanza hadi wa tatu walioshiriki mashindano ya Boti
zinazokwenda kwa upepo (Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 baada ya
kukabidhiwa vikombe na zawadi zao yaliyofanyika katika fukwe za Yatch
Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo
yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)