Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Rufiji, Dk. Seif Rashid (Kulia) akisalimiana na akina mama wa Kijiji
cha Mtanza baada ya kumalizika kwa mkutano na wananchi wa eneo hilo
wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge
pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Dk Rashid akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtanza jimboni humo juzi
Mkazi wa Kijiji cha Mtanza, Yusufu Nyamgumi, akihoji kwenye mkutano
kitendo cha Diwani wao, Athuman Mbange (CUF) kutokuwa na tabia ya
kuwatembelea kujua matatizo yao.
Bibi
Fatuma Mazengo akilia wakati akisimulia namna mtoto wake na mjukuu
wake walivyo uwawa kikatili na Askari wa Wanyamapori katika mpaka wa
hifadhi ya Selou maeneo ya Mloka, Rufiji. watu hao wanadaiwa kuuwawa
wakati walipokwenda kuvua samaki katika ziwa Mzizizmia.
Akina mama wa Kijiji cha Mibuyu Saba wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Rufiji, Dk. Seif Rashid (wa pili kukushoto) akiwa na baadhi ya viongozi
wa Kata ya Mwaseni, akikagua maendeleo ya ujenzi wa chumba cha darasa
wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na
kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya Unaibu Waziri.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)