USAILI kuwania nafasi
ya uongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA), umefanyika
mapema leo Agosti 22, chini ya Mwenyekiti wake Dr. Haule na kushuhudia
viongozi mbalimbali wakichaguliwa huku mdau wa michezo na aliekuwa
Mjumbe wa Villa Squad, Ally Kindoile, kupenya kwenye usaili huo.
Katika usaili huo ulioshuhudiwa
na wadau mbalimbali wa michezo, ulifanyika katika ofisi za Manispaa ya
Moshi, ambapo nafasi ya Mwenyekiti waliopita ni pamoja na Godluck Moshi
na Charles Mchau, Makamu Mwenyekiti Shaban Mwalimu na nafasi ya
Katibu Mkuu msaidizi kwenda kwa Ally Kindoile.
Aidha nafasi zingine walizopita
wadau hao wa soka wa Mkoa wa Kilimanjaro, majina na nafasi zao kwenye
mabano ni Kusianga Kiata (Mhani), Distin Kilua na Abdala Husein
(Wajumbe Mkutano Mkuu).
Wengine ni Keneth Essau na Amri
Kiula (Wawakilishi wa Vilabu), Denis Joseph Msemo, Cuthbert Mushi na
Nassor Muchi (Wajumbe Kamati ya utendaji) na Salma Omari Mndaira
(Mwakilishi TWFA).
Katika hatua hiyo, Uchaguzi wake unatarajia kufanyika Septemba 9,Ulili, Mkoani humo.
Hata hivyo, Ali Kindoile
alipozungumza na waandishi wa Habari, muda mfupi baada ya usaili huo,
alishukuru kwa kupita kwake na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano
katika kuinua soka la Mkoa huo, ambapo mipango yake mbalimbali
anatarajia kushirikiana na wagombea wenzake pindi watakapofanikiwa kwa
pamoja kupata nafasi hiyo hiyo Septemba 9.
“Tunaomba ushirikiano na umoja ili kufika mbali katika soka letu, umoja wetu ndio tutasaidia soka la mkoa huu” alisema Kindoile.
Kindoile licha ya kuwa mdau wa
michezo, aliwahi kuchezea timu mbalimbali zikiwemo Simba B na Idrisa Fc,
kwa sasa ni mdau mkubwa wa timu ya Kilimanjaro Rangers ya mkoani humo
na amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia vijana kwenye soka.
Uchaguzi huo awali ulitakiwa kufanyika Agosti 28, ambapo sasa umesogezwa mbele mpaka hapo Septemba 9.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)