Mama Maria Nyerere Akabidhi Matrekta 10 Kwa Kijiji Cha Kwadelo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mama Maria Nyerere Akabidhi Matrekta 10 Kwa Kijiji Cha Kwadelo

 Mama Maria akimkabidhi funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
 Mkazi wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za Matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa kijiji hicho  kilichopo wilayani Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo, katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati.
 Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
  Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama
  Kariati akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mama Nyerere
 Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Maria Nyerere, akimkaribisha, diwani wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya KLondoa mkoa wa Dodoma, Alhaj Omar Kariati, wakati diwani huyo na ujumbe wake wa wakulima kumi, walipofika nyumbani kwa Mama Nyerere kwa ajili ya kukabidhiwa trekta kumi kwa wakulima hao, katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam, jana. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages