Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi kikombe Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Salum Ally,
baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa mshindi wa jumla katika
maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo, wakati
alipokuwa akifunga maonyesho hayo katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima,
wakati alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima
Nanenane yaliyomalizika leo, katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati
walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo, kwa ajili ya
kufunga rasmi maonyesho hayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete, kufunga
rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo,
katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa
ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na kuendeleza
Kilimo Kwanza, wakati Makamu alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya
Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma
leo. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher
Chiza.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)