Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala wakisimamiwa na Kocha wa mchezo uho Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' jana Class anajiandaa kupambana na Sako Mwaisege ' Dunga' siku ya Idi pili katika Ukumbi wa Diambond Jublee na Sunga anajiandaa kupambana na Mussa Seif 'Boda boda' katika Uwanja wa Bandari Tandika Dar es salaam
Mabondia
Mussa Sunga kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakioneshana
umwamba wa kutupiana masumbwi wakati wa mazoezi yao ya kujitaalisha na
mapambano ya ngumi siku ya Idi pili Sunga atacheza na Mussa Seifu 'Boda
boda katika uwanja wa Bandari na Class atapambana na Sako Mwaisege
'Dunga' katika ukumbi wa Diamond Juble KAMBI YA NGUMI ya Ilala jijini Dar es salaam ipo katika mazoezi ya kuwaandaa mabondia wake wawili watakaopanda ulingoni siku ya Iddi pili katika viwanja viwili tofauti Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi anaesimamia Kambi ya Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia hawo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Mussa Sunga aliongeza kwa kusema kuwa mpambano wa Sunga litafanyika katika uwanja wa Bandari Tandika Dar es salaam na atazichapa na Mussa Seif 'Boda Boda' siku ya Idd pili na bondia Class atapanda ulingoni siku hiyo hiyo katika ukumbi wa Diamond Jublee kuzipiga na bondia Sako Mwaisege 'Dunga' aliongeza kwa kusema mabondia hawo wapo katika mazoezo mazito wakisimamiwa na yeye mwenyewe na kocha mkongwe wa mchezo huo Habibu Kinyogoli 'Masta' pamoja na Kondo Nassoro Katika michezo hiyo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo, Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia, makocha waamuzi pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali. ''Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na Mtanzania Roja Mtagwa anayefanya shughuli zake Marekani. “DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi,'' alisema Super D. DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi Ilala na klabu ya Ashanti ya Ilala hapa Jijini. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)