Kituo cha Kisasa cha NHIF kitaboresha huduma-Waziri - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Kituo cha Kisasa cha NHIF kitaboresha huduma-Waziri

  Meneja wa Kanda ya Kati wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Daudi Bunyinyiga akitoa maelezo ya mradi wa Kituo cha Matibabu cha Kisasa kinachojengwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma, kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alipotembelea mradi huo.
Naibu Waziri akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Hospitali hiyo.
 

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa kukamilika kwa mradi wa Kituo cha Kisasa cha Uchunguzi wa Magonjwa unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Chuo Kikuu Dodoma utapunguza utegemezi wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa kuwa kitakuwa na vifaa vya kisasa na madaktari bingwa.


Hayo yalisemwa na Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka wakati akijibu hoja ya Kambi ya Upinzani ambayo ilihoji faida za uwezekezaji unaofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika Chuo Kikuu cha Dodoma.


“Uwekezaji katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Medicare Centre of Excellence) ni eneo mojawapo linalolenga kuhakikisha kuwa huduma za rufaa nchini zinaimarika ikiwemo kupunguza utegemezio wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi,” alisema Waziri.


Alisema kuwa mradi huo utakuwa na huduma muhimu kwa wanachama na wananchi kwa ujumla ikiwemo huduma za matibabu ya figo, huduma za vipimo muhimu kama Magnetic Resonance Imaging (MRI) na vipimo vingine vya uchunguzi.


Aidha kituo hicho cha kisasa kitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wanaosomea shahada ya udaktari kujifunzia kwa vitendo.


Waziri Kabaka pia litumia fursa hiyo kufafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria ya Mfuko huo kifungu cha 33b kinauruhusu Mfuko kuwekeza katika vitega uchumi ambavyo vinalenga moja kwa moja uboreshaji wa huduma za afya nchini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages