Beatrice
Shimende Kantimbo (48) anaomba msaada wa pesa kwa ajiri ya matibabu ya
maradhi ambayo vipimo vya kitabibu vimegundua kuwa ni matende
(elephantiasis), ili kufanikisha safari yake kwenda India kwa matibabu.
Kantimbo
anasumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miaka 12, kwahivi sasa
yamemtoa kwenye mstari wa maisha yake ya kujitegemea na kumfanya awe
tegemezi kwa watoto wake na mumewe ambao hata hivyo kipato chao si cha
uhakika.
Kabla
ya hapo alikuwa ni mama 'mchakarikaji' kweli, aliendesha maisha yake
kwa biashara kadhaa ikiwemo biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi
wa nywele ambapo yeye mwenywe ni msusi mzuri wa nywele na kwa ucheshi
wake na kujiamini pia alikuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC) kwenye
sherehe kadhaa akifahamika kama MC Kimbaumbau.
Ila
kwa sasa, tofauti na hapo awali alipoitwa MC na mama mchakariji,
Kantimbo hawezi kufanya lolote amebakia ni mama wa kukaa mahali pamoja
tu kuanzia asubuhi hadi jioni.
Kwa
uchungu anasimulia namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa
kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa
(anaonyesh pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo
hayakudumu sana wala hapakuwa na alama yoyote.
"Baada
ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka mwili mzima,
nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali
nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua nilikuwa
na malaria.
"Wakati
huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha. Malaria
ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali.
Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu
unavimba. Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"
Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka kuvimba
na maumivu makali yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na
kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza.
Anasema:
"Baadhi
ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali kukatwa mguu. Wanasema
ya nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi sikukukubaliana na
ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007 iligunduliwa tatizo
kubwa lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji kutokana na
nyama kuharibika. Sio mfupa.
"Nilikataa
kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa kusimama na
kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu
zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto" alisema.
Kwa mawasiliano namna ya kumsaidia piga simu namba 0716 850350, 0784 861031.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)