Kocha mpya wa timu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Pablo Ignacio Velez kutoka Argentina wa kwanza kulia, akizungumzia nini atafanya akiwa na
timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao uliopangwa kuanza Septemba Mosi mwaka
huu. Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo. Wengine
katika picha ni Charles Otieno ambaye ni mkurugenzi wa ufundi na
Biashara wa timu hiyo.
****
Mwandishi wetu
KOCHA mpya wa timu ya soka ya African Lyon, Pablo Ignacio Velez, amewasili nchini tayari kuanza kuinoa timu hiyo na kuomba apewe muda wa kukisuka upya kikosi hicho huku akiahidi mabadiliko zaidi ya soka kwenye timu hiyo.
KOCHA mpya wa timu ya soka ya African Lyon, Pablo Ignacio Velez, amewasili nchini tayari kuanza kuinoa timu hiyo na kuomba apewe muda wa kukisuka upya kikosi hicho huku akiahidi mabadiliko zaidi ya soka kwenye timu hiyo.
Pablo
raia wa Argentina aliyasema hayo jana baada ya kusaini mkataba wa mwaka
mmoja kuitumikia timu hiyo na kusisitiza lengo lake kubwa ni
kuhakikisha vijana wanapewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na ndivyo
itakavyokuwa Afrika Lyon.
"Sikuja
Tanzania kutafuta pesa, ndoto yangu kubwa ilikuwa kufundisha soka
barani Afrika hivyo wakati ni sasa," alisisitiza kocha anayezungumza
lugha ya 'kiispanyola'.
Pablo
alisema "kazi ya aina yoyote lazima ipewe muda na mchezaji lazima
atengenezwe hivyo watanzania wawe na subira kwa ajili ya kupata matunda
mazuri ya vijana hapo baadae kutoka African Lyon.
Kocha
huyo aliyewai kuzichezea timu za taifa za vijana chini ya miaka 17 na
20 za Argentina hakusita kusisitiza suala la nidhamu kwa wachezaji wa
timu hiyo ya ndani na nje ya uwanja.
"Nidhamu
ni muhimu kwa wachezaji wangu cha msingi tushirikiane katika
kufanikisha hili kwa vijana kwani mchezaji anatakiwa kati ya miaka 18 na
19 awe ametengeneza jina kupitia soka ," alisema Pablo.
Naye Mmiliki wa African Lyon, Rahmu Kangezi alisema lengo la kumleta kocha huyo ni kuhakikisha timu hiyo inajongea mbele zaidi.
Kangezi
alisema licha ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja lakini wanaweza
kumtumia Pablo kwa kipindi kirefu kulingana na mfumo wa kuhakikisha
wanaendeleza vijana katika timu yao.
"Pablo
ni zaidi ya kocha, ana uwezo pia amecheza mpira pia ni kocha wa kwanza
kutoka Argentina kuja Tanzania hivyo tunaimani timu yetu ya African Lyon
itafika mbali zaidi kisoka," alisitiza Kangezi.
Pablo mwenye miaka 38 aliyechukua mikoba iliyoachwa na Jumanne Chale amewai kuifundisha klabu ya Atletico Colo Colo De Chile (1998).
Pablo mwenye miaka 38 aliyechukua mikoba iliyoachwa na Jumanne Chale amewai kuifundisha klabu ya Atletico Colo Colo De Chile (1998).
Klabu
nyingine alizowai kufundisha ni Atletico Calchin (2000), Atletico
Belgrano De Cordoba (1997), Atletico River Plate (1993-1995).
Klabu
nyingine ni Banco De Cordoba (1991 na 1997), Deportivo Lasallano (1992)
Atletico Argentino Penarol kwa miaka minne na klabu nyingine nyingi za
Hispania na Argentina.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)