Kamishina wa Idara ya Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya Bw. Danford Makala (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Ustawi wa jamii wakati wa mkutano kati ya Ujumbe wa
Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland na
watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jana jijini Dar es
salaam.
Meneja Mkuu na mmiliki wa Hospitali zinazojengwa kwa kutumia makontena (Hospitainer) na kuweza kupelekwa kutoa huduma za afya maeneo yoyote kutoka
nchini Netherland Bw. Rolof Mulder akiongea na watendaji wa wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii kuelezea namna kampuni hiyo inavyofanya kazi
zake.
Baadhi ya viongozi wa ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland wakifuatilia
fafanuzi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na watendaji wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii jana jijini Dar es salaam.
Watendaji
wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya
pamoja na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka
nchini Netherland
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)