Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA), Esther Abayo akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana kuhusu uzinduzi wa kampeni maalum kwa ajili ya
ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike katika Shule za Sekondari nchini
utakaofanyika tarehe 14 Julai Kibaigwa mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja
Habari Elimu na Mawasiliano, Sylvia Lupembe.
Meneja Habari Elimu na Mawasiliano wa
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe akifafanua jambo kuhusu
uzinduzi wa kampeni maalum kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi
wa kike katika Shule za Sekondari nchini utakaofanyika tarehe 14 Julai
Kibaigwa mkoani Dodoma. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA), Esther Abayo na Mkurugenzi wa Uhamasishaji
Rasilimali Watu, Seif Mohamed.
Mkurugenzi
wa Uhamasishaji Rasilimali Watu, Seif Mohamed akifafanua jambo kuhusu
uzinduzi wa kampeni maalum kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi
wa kike katika Shule za Sekondari nchini utakaofanyika tarehe 14 Julai
Kibaigwa mkoani Dodoma. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA), Esther Abayo.
--
Mamlaka
ya Elimu Tanzania inatarajia kuzindua kampeni kwa ajili ya ujenzi wa
hosteli za wanafunzi wa kike katika shule za sekondari nchini tarehe 14
Julai 2012.
Uzinduzi
huu utafanyika mkoani Dodoma katika mji mdogo wa Kibaigwa ambapo mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh.
Philip Mulugo(Mb). Pia uzinduzi huu utahusisha viongozi mbalimbali wa
serikali, wabunge, Wadau wa elimu, wakazi wa eneo hilo, wazazi na
wanafunzi wa shule ya sekondari Kibaigwa na zingine zilizo jirani.
Katika
Kampeni hii Mamlaka inalenga kujenga hosteli 30 kupitia michango ya
wadau mbalimbali. Kiasi kinacholengwa ni shilingi za kiatanzania 2.3
bilioni ambapo kila bweni litagharim shilingi millioni 78 bila samani.
Jumla ya wanafunzi wa kike 1,504 watahudumiwa pindi ujenzi wa hosteli
hizi utakapokamilika.
Shule
za sekondari zitakazofaidika na mradi huu ni Ufana - Manyara, Mibukwe -
Tanga, Kibaigwa - Dodoma, Milola - Lindi, Nyihara - Mara, Lundo -
Ruvuma, Butundwe - Mwanza na Buseko hill – Kigoma.
Serikali
kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu inakusudia kujenga hosteli 100
katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya wanafunzi wa kike 4,800
ifikapo mwaka 2015. Kutokana na wingi wa shule za sekondari nchini na
ongezeko la mahitaji ya hosteli ndipo Mamlaka ikaamua kuongeza nguvu
juhudi hizo kwa kushirikisha jamii kuchangia fedha na rasilimali
nyingine ili kujenga hosteli hizo 30 ambazo ni asilimia 30 ya azimio la
serikali.
Dhamira ya Mamlaka ya Elimu Tanzania kujikita katika suala la hosteli kwa wanafunzi wasichana wa sekondari ipo
katika mpango mkakati wake (ROLLING CORPORATE STRATEGIC PLAN 2010/11 –
2014/15) ambapo kwa awamu ya kwanza imedhamiria kujenga hosteli 30.
Changamoto
za ukasefu wa hosteli kwa wanafunzi wa kike wanaotokea nyumbani au
waliopanga ni pamoja na muda mchache wa kujisomea kwani wanalazimika
kutimiza majukumu ya nyumbani kabla ya kuanza kujisomea, vishawishi na
udhalilishaji wakiwa njiani wakielekea shuleni, wale waliopanga nyumba
za karibu na shule wanajikuta wakitumia muda mwingi kutafuta maji na
chakula na pia wanajikuta wakiwa katika ushawishi mkubwa wa kuingia
katika mapenzi wakiwa na umri mdogo, hali inayopelekea kupata mimba na
hivyo kukatisha masomo
Takwimu
za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi .(MoEVET Best, 2011) zinaonesha
wanafunzi wa kike 16,656 walifukuzwa shule kutokana na mimba kati ya
mwaka 2008 na 2010. Wakuu wa
shule wamashauri kwamba tatizo hilo linaweza kupunguzwa iwapo wanafunzi
wa kike watapatiwa makazi bora na salama katika maeneo ya shule.
Tunawaomba wadau wa Elimu na watanzania kwa ujumla kuchangia katika kampeni
hii kwa fedha taslimu au vifaa kama vifaa vya ujenzi au samani za
hosteli. Kwa michango ya fedha taslimu unaweza kuchangia kwa kutuma
fedha katika akaunti ya Mfuko iliyopo benki ya CRDB 01J1027639900, au
kwa kupitia akaunti ya M-pesa namba 404040 Unaweza pia kuwasilisha
mchango wako katika ofisi za Mamlaka ya Elimu Tanzania zilizopo
Mikocheni barabara ya kambarage au katika vituo vya televisheni vya ITV,
channel ten na star TV
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)