WANAFUNZI WAWILI KUTOKA UN CLUBS KUIWAKILISHA TANZANIA KONGAMANO LA MANDELA AFRIKA KUSINI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WANAFUNZI WAWILI KUTOKA UN CLUBS KUIWAKILISHA TANZANIA KONGAMANO LA MANDELA AFRIKA KUSINI

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot, akimkabidhi barua Mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Azania,  Rahim Rajab ambaye ni mmoja wa kati ya wanafunzi wawili wajumbe wa UN Clubs waliochaguliwa kuhudhuria Kongamano la maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, litakalofanyika Johannesburg Afrika Kusini ambayo huadhimishwa kila mwaka Julai 18.
Wanafunzi hao wamepewa udhamini wa Tiketi za kwenda na kurudi na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways-SAA).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot, akimkabidhi barua ya kuchaguliwa kushiriki Kongamano hilo Afrika Kusini Mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa,  Nuru Kessy, ambaye ni Mwanachama wa Un Clubs.
Bw. Phillippe Poinsot (kulia) akimfafanulia Mwanafunzi Nuru Kessy, kuwa katika Kongamano hilo watakutana na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali duniani wenye umri kati ya miaka 13-18 na kuwa wanahitaji kufanya utafiti kuhusiana na maisha ya Mandela ikiwemo miaka ya mwanzo, maisha yake ya jela, maisha ya uraisi kama mtu aliyepokea tuzo ya Amani ya Nobel, kustaafu kwake na mchango wake kama kiongozi maarufu duniani.
Wanafunzi hao wakitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot (kulia) na Head, Management Support Strategy and Partnership wa UNDP Ishmael Dodoo (kushoto).
Wanafunzi ambao ni wananchama wa UN Clubs wanaoelekea Afrika Kusini katika Kongamano la maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Nelson Mandela kwa udhamini wa shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa UNDP. Kushoto ni Reference Assistant kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Harriet Macha, IT Associate Alice Chopeta, Head, Management Support Strategy and Partnership wa UNDP Ishmael Dodoo, Wanafunzi Rahim Rajab na Nuru Kessy, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot na Information Officer UNIC Stella Vuzo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages