Na Mwandishi Wetu Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’
Bendi kongwe nchini Msondo Ngoma Music na Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae”
zinatapambana kesho Ijumaa kuanzia saa moja usiku kwenye ukumbi wa Klab Lazizi Dodoma.
Pambano
hilo ambalo tayari limevuta hisia za mashabiki wa muziki wa dansi
nchini ikiwemo wabunge
imeandaliwa kwa ajili ya kujua nani zaidi baada ya mwaka jana kuwa na
utata wa nani zaidi ambapo kila mmoja alikua anadai yeye ni zaidi.
Akizungumza na waandishi wa Habari Msemaji wa Bendi Ya Msondo ngoma Rajabu Mhamila Super D' alisema
Onyesho
hilo pia ni maalum kwa ajili ya kuwaaga mashabiki wao kwa kuwa tunaelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani
ambapo wapenzi wa muziki watajumuika kwa pamoja kwenye Ukumbi huo hivyo
kufurahia
Bendi
hizo ambazo zina mashabiki wengi nchini kuliko bendi nyingine zozote,
zimeahidi kutowaangusha mashabiki wao kwa kila moja ikijinasimu kuwa
itaibuka na ushindi.
Mara
nyingi bendi hizo zikipambana huwa ni patashika nguo kuchanika, kwani
mbali na mashabiki kushangilia bendi wanazozipenda vibweka na vituko
kemkem vimekuwa vikitawala.
Sikinde ambayo iliweka kambi jijini Dar es Salaam imejinasibu kuibwaga Msondo na kudai kuwa hivi sasa haitishi kama ile ya miaka kadhaa iliyopita.
Itakuwa ni mara nyingine tena kupambana
katika pambano hilo mbali na kuwakumbuka wanamuziki wao waliofariki,
lakini pia itakuwa ni kusherehekea miaka 50 ya Uhuru huku zikiwa bado
zinadumu kwani bendi nyingi za rika lao zimeshafutika kwenye ramani ya
muziki nchini.
Sikinde inayongozwa na Habibu Jeff uku Msondo ikiongozwa na Mkongwe wa muziki nchini Muidini Gulumo.
Tunataka mashabiki wa bendi zote wajitokeze kwa wingi bila ya kuwa na wasiwasi kwani
watapata burudani ya kutosha , kwani watapiga zile nyimbo za
zamani wakati bendi hiyo inaanzishwa mwaka 1978 kama vile 'Selina',
Wiki endi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi namba 1 na 2 hadi za
kisasa kama vile 'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.
Naye kiongozi wa Msondo Said Mabera maarufu kama Doctor amesema kuwa kama kawaida yao Msondo ni bendi isiyoshindwa daima.
Mabera amesema kuwa siri ya bendi hiyo kupata ushindi miaka yote ni ushirikiano wanaoupata wanamuziki na wapenzi wao.
Wamewataka
wapenzi wao kama kawaida yao kujitokeza kwa wingi na kuishangilia kwa
nguvu Msondo Ngoma kwani itaporomosha vibao vya enzi za Nuta, Juwata,
Ottu hadi Msondo Ngoma.
Baadhi
ya nyimbo zao ni 'Nimuokoe nani', 'Zarina', 'Mwanaidi',
'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif',
'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali',
'Suluhu' na nyingine nyingi.
Kikosi
cha Sikinde kitakuwa na Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata,
Kaingilila Maufi, Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma
Choka, Ally Jamwaka, Athumani Kambi, Mbaraka Othman, Milambo, Shaaban
Lendi, Joseph Benard na Ramadhani Mapesa.
Msondo
itawategemea akina Shaaban Dede alijiunga hivi karibuni kutoka
Sikinde, Mabera, Abdul Ridhiwani Pangamawe, Saad Ally 'Mashine', Eddo
Sanga, Huruka Uvuruge, Zahor Bangwe, Ibrahim Kandaya, Ismail Mapanga,
James Mawilla, Muhidini Gurumo, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hamisi
Mnyupe, Roma Mng’ande `Romario’ na Hassan Moshi.
Aidha Super 'D' alimariza kwa kutaja
ratiba yao ya wiki hii kuwa jumamosi watakuwa Kibaha Kontena kwa ajili
ya kuwapa burudani mashabiki wake na watamaliza wikiendi katika ukumbi
wa Dar Live uliopo Mbagala Dar es salaam siku ya jumapili hivyo wapenzi
wajitokeze kwa wingi ili wapate burudani
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)