Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
WAZIRI
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara,
amemteua Dkt. Selemani Sewangi (55) kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la
Kiswahili la Taifa (BAKITA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa wizara hiyo, uteuzi huo umeaanza rasmi Julai Mosi mwaka huu.
Taarifa
hiyo ilifafanua kuwa Dkt. Sewangi ni Mhadhiri Mwandamizi wa Taasisi za
Kiswahili (TATAKI) kutoka Chuo Kikuu cha Dares Salaam.
Dkt. Sewangi anachukua nafasi hiyo iliyoachwa na Dkt. Anna Kishe, aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)