WASHINDI WENGINE WANNE WASHINDA ZAWADI ZA SBL,WAWILI WASHINDA GENERETA, MMOJA AJISHINDIA PIKIPIKI,HUKU MWINGINE AKIJINYAKULIA BAJAJ, ZAWADI ZOTE MPYA KABISA,
Meneja wa bia ya
Serengeti Lager Bw. Allan Chonjo wa pili kutoka kulia akiwasiliana na
mshindi katika bahati nasibu ya Vumbua Dhahabu chini ya kizibo
inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti, Kulia ni Meneja
mawasiliano wa SBL Imani Lwinga na kutoka kushoto ni Cheryl Vroom kutoka
PWC, Tumainieli Malisa kutoka PWC na waliosimama nyuma kulia ni Joyce
Mwijage Mratibu Rasilimali watu SBL na Abubakary Maggid kutoka Bodi ya
michezo ya kubahatisha.
Ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL.
Kampuni ya bia ya Serengeti leo
imeendelea na droo ya tisa katika promosheni inayoendelea ya ‘VUMBUA
HAZINA CHINI YA KIZIBO’ iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo SBL
zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kuhudhuriwa na waandishi wa
habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka
ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati
Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House
Coopers.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia
vinywaji vyake aina ya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner
Lager inaendesha promosheni hiyo nchi nzima ambapo kwa mara nyingine
washindi wane wameweza kuibuka na ushindi katika droo iliyochezeshwa leo
asubuhi.
Akionge na wandishi wa habari wakati wa
kuchezesha droo hiyo, meneja wa bia ya serengeti lager bw. Allan Chonjo
amesema “ni wiki ya tisa sasa ambapo tunaendelea na promosheni yetu
ambayo
bila shaka watanzania wengi mmekuwa mkishuhudia watanzania wenzenu
wakijishindia zawadi mbalimbali nakukabidhiwa pale walipojipatia zawadi
hizo’ naendelewa kuwasisitiza wateja wetu na watatnzania wote kwa ujumla
kuwa bado zawadi zipo nyingi na kwambakila mmoja wenu anaweza kushinda
kama vile ambavyo wengine wanajishinadia
Washindi wetu katika droo hii ya tisa ni
bwana Boaz Mtukula kutoka Mwanza ambaye ni mfanyakazi wa benki ya Twiga
Bancorp mywaji wa bia ya Tusker Lager na bwana Richard Valerian kutoka
Dar Es Salaam anayefanya kazi Bandarini mywaji wa Tusker pia ambao wote
kwa pamoja wamejishindia jenereta mapya kabisa, na bibi Rahma Ally mkazi
wa Temeke jijini Dar Es Salaam ambaye amejinyakulia pikipiki
mpya mywaji wa bia ya Serengeti Premium Lager na Bwana Richard Mbizi
mkazi wa Kimara jijini Dar Es Salaam amamejishindia bajaj mpya kabisa,
zawadi zote kutoka SBL
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)