Timu ya Tanzania ya Olimpiki, imewasili kwenye
kijiji cha michezo ya Olimpiki kilichopo Stratford, London, ikitokea
kwenye mji wa Bradford. Timu hiyo ya Tanzania, iliweka kambi ya mazoezi
katika Chuo Kikuu cha Bradford tangu walipowasili nchini Uingereza wiki
mbili zilizopita, ikiwa tayari kuiwakilisha Taifa katika michezo hiyo
ya Olimpiki 2012. Timu hiyo ilipokelewa na Balozi wa Tanzania, nchini
Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe na maofisa wengine wa Ubalozi na
kusindikizwa moja kwa moja kwenye kijiji cha michezo hiyo kilichopo
Stratford, ikiwa tayari kwa maandalizi na ufunguzi rasmi wa michezo hiyo
utakaofanyika siku ya Ijumaa 27/07/2012 hapa London.
Pichani, Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Peter
Kallaghe akiwa pamoja na Wanamichezo hao watakaoiwakilisha Taifa mwaka
huu katika Michezo hiyo ya Olimpiki nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)