Afisa
sera na utafiti CHADEMA Makao makuu, Waitara Mwita akifurahi na
wanachama wa CHADEMA, baada ya kupata dhamana mjini Singinda
Mwita Waitara akizungumza na wanahabari mjini Singida baada ya kuwekewa dhamana ya wadhamini wawili
Mwita
Waita (wa kwanza kushoto), akifurahi na wafuasi wa CHADEMA mahakamani
mjini Singida, baada ya kupata dhamana ktk kesi ya mauaji.
VIJANA
sita, Watuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti UVCCM Yohana Mpinga wa Kata
Ndago Iramba Singida, wakipandishwa kwenye gari la polisi.Picha na Habari na Elisante John
--
WATU
sita wamepandishwa kizimbani Mjini Singida, kujibu shitaka la mauaji
ya Mwenyekiti UV-CCM Kata ya Ndago Wilaya Iramba,Yohana Mpinga, katika
vurugu zilizohusisha wafuasi wa CHADEMA na CCM.Wamesomewa
shitaka hilo na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Neema Mwanda
mbele ya hakimu mfawidhi mahakama ya Mkoa Singida, RuthMassam.
Walioshitakiwa ni
Manase Daudi (40), Williamu Elia (33), Frank Stanley (20), Charles
Leonard (36), Tito Nintwa na Fillipo Edward (30), wakazi wa Ndago,
Wilaya Iramba.
Wamedaiwa kufanya kosa hilo Julai 14, 2012 saa kumi alasiri, katika kijiji cha Nguvumali, kwa kutumia mawe na fimbo.
Hawakutakiwa kujibu lolote, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo na itatajwa tena Julai 30, 2012.
Pia kesi
nyingine iliyosomwa na mwanasheria wa Serikali Seif Ahmad,
imemhusisha afisa sera na utafiti wa CHADEMA makao makuu Waitara Mwita
(37) mkazi wa jijini Dar-es-salaam, akidaiwa kutoa lugha ya matusi
mkutanoni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)