Mratibu
na jaji wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa
2012,Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali kutoka Clouds FM,akimpa maelekezo
mafupi Pacha Great mara baada ya kuibuka kinara wa shindano la kumsaka
mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,kwa kuwashinda mahasimu wenzake
wapatao 32 waliofika kushirika mchakato wa shindano hilo.shindano la
kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa limeandaliwa na Prime Time
Promotions/Clouds FM kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya bia ya Serengeti
kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
Wasanii
chipukizi walioshiriki shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc
Shujaa,kutoka kulia ni Pacha Great akimchana live kwa kughani msanii
mwenzie aitwaye Chalz Gibson wakati wa shindano hilo,ambpo Pacha
aliibuka mshindi na kuwa mshindi wa shindano la kumsaka mkali wa
Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012 ndani ya jiji la Arusha.
Mmoja
wa majaji wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc
Shujaa,Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali akifafanua jambo kwa washabiki na
watazamaji mbalimbali waliofika kwenye shindano hilo ndani ya ukumbi wa
Mawingu Club,mjini Arusha mapema jana jioni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)