Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa
Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa
Veta mjini Dodoma leo. Katikati ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin
Shaaban Simba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya waumini na viongozi wa Jumuiya za Kiislamu wakati
akiondoka, baada ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza
Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta
mjini Dodoma leo.
Baadhi
ya Viongozi wa Jumuiya za Kiislamu na waumini wa Dini hiyo,
waliohudhuria semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam
Tanzania (BAKWATA) iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, iliyofanyika kwenye
Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)