LEKA
DUTIGITE KIGOMA.. ni tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika mkoani
Kigoma tarehe 17 ndani ya mwezi huu wa saba na kuwashwa moto na wasanii
wazawa wa kigoma. Mpaka sasa ari waliyonayo wasanii hao ni ya kubwa
mno.. mpaka imekuwa kama ni changamoto kwa wasanii wanaotoka katika
mikoa mingine, na kulowea zaidi Dar es Salaam.
Hata
hivyo breaking news inaonyesha kuwa karibia nusu ya nyimbo zinazofanya
vizuri hivi sasa katika soko la muziki hapa nchini ni za wasanii
wanaotoka katika mkoa wa kigoma. Angalia nyimbo kama "Kichwa kinauma"
yake Ali Kiba aliyomshirikisha Jaydee, "Upepo" Recho, "Mawazo" Diamond,
"Maneno maneno" Queen Darleen, "Jua ni wewe" Mwasiti akimshirikisha Ally
Nipishe, Na nyingine nyingi kutoka kwa wasanii wao kina Chege, Abdu
Kiba, Baba Levo, Makomandoo Bongo, Linex, Banana Zorro na wengine wengi.
Jambo
lingine la kutia hamasa ni jinsi Mbunge wao wa Kigoma Zitto Kabwe
anavyoshirikiana nao katika kila jambo. Naye msimamizi wa ama mratibu wa
tamasha hilo Mwasiti Almas naye alifunguka na kusema haya "Kila kitu
kwetu kama wasanii wa Kigoma kiko tayari kwa ajili ya tamasha hili,
Kilichobaki ni wasanii wenyewe kufika mkoani kwao na kutimiza lengo la
Tamasha hili, kwani tamasha hili linasimama kuwatia chachu ama hamasa
vijana wa mkoa wa Kigoma mkoani humo".
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)