MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL
|
Cables: "MUHIMBILI" Postal Address:
Telephones: 255-22-2151367-9 P.O. BOX 65000
Fax: 255-22-2150234 DAR ES SALAAM
Web: www.mnh.or.tz TANZANIA
MADAKTARI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI WAREJEA KAZINI
JULAI 2, 2012
Huduma
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida
baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.
Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara
ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu
wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za
tiba zimefanyika kama kawaida.
Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16,
kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar
watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo
Upande
wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja
yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.
Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.
Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.
Kuhusu
huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi
ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji
haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa
upasuaji..
KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.
Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 1, 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)