KATIBU
Mkuu wa CCM, Wlson Mukama, akizawadiwa na kiongozi wa ujumbe wa Chama
Cha Kikomusti cha China, Ma Wen baada ya mazungumzo yao.
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Wilson Mukama, akizungumza na
ujumbe wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Ofisi Ndogo ya Makao
Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, Jana.Ujumbe
huo unaongozwa na Ma Wen (wa pili kulia), ambaye ni Naibu Katibu wa
Tume ya Taifa ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC. Wajumbe wengine na vyeo vyao
katika mabano ni Keng Xiangren (Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Usimamizi), Tian Chengjiang (Mkurugenzi wa
Taasisi ya Usimamizi katika Mkoa wa Ning Xia), Ding Bodong (Mkurugenzi
wa Usimamizi katika jimbo la Hai Nau), Dai Hui (Naibu Mkurugenzi wa
Idara ya Utawala katika Wizara ya Usimamizi) na Cai Wei, ambaye ni Mkuu
wa Sehemu ya Idara ya Uhusiano wa Kimataifa katika wizara hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)