MAHEKALU YA VIGOGO DAR YABOMOLEWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAHEKALU YA VIGOGO DAR YABOMOLEWA

Hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa tamko la Makamu wa Rais la mwaka 2004 ambalo lilitaja maeneo tengefu ambayo yalipaswa kuhifadhiwa zikiwamo fukwe za bahari ambazo zina mikoko ambayo ni mazalia ya samaki baharini. Licha ya tamko hilo na sheria mbalimbali, bado maeneo ya fukwe za bahari yamekuwa yakivamiwa.

Katika kusimamia sheria na tamko hilo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kitengo cha Hifadhi ya Misitu, Baraza la Taifa la Kuhifadhi Mazingira (NEMC) na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, ziliamua kuratibu bomoabomoa hiyo ya nyumba za kifahari zilizojengwa maeneo tengefu ya bahari.

Bomoabomoa hiyo ambayo iliendeshwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wa FFU chini ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela na kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa NEMC, Dk Robert Ntakamulenga, jumla ya nyumba 27 kati ya hizo 15 zikiwa zimekamilika ujenzi, nane uzio (fence) na nyingine katika hatua za awali za ujenzi, zilibomolewa.

Kazi ya kubomoa nyumba hizo iliyofanywa na kampuni ya Majembe Auction Mart, ilianza huku wakazi wa nyumba hizo wakiwekwa chini ya ulinzi mkali wa FFU na polisi wengine waliokuwa wamesheheni mabomu ya machozi, bunduki na gari la kumwaga maji ya kuwasha.

Bomoabomoa hiyo ilianzia katika eneo la Hifadhi ya Mikoko, Mbezi Beach mnamo saa 2:00 asubuhi na watu waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo walilazimika kutoa vitu vyao nje huku kububujikwa machozi.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo na Mchungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Christian, George Makala alisema kitendo hicho kinasikitisha kwa kuwa muda uliotolewa kwao ni mdogo na wasingeweza kujiandaa kuhama.

Akizungumzia tukio hilo muda mfupi baada ya kubomolewa nyumba yake na kanisa hilo, Mchungaji huyo alisema kitendo hicho hakikufuata taratibu na kimesababisha hasara ya mali nyingi kwa wakazi wa eneo hilo akisema kama wangeachwa wahame zingeokolewa.

“Ninasikitika sana kwani kitendo hiki hakikufuata taratibu, alikuja Waziri wa Nyumba, Ardhi na Makazi Profesa Anna Tibaijuka, Mbunge wetu, Halima Mdee na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda wakatuambia eneo hilo siyo la hifadhi, bali ni hatarishi, sisi tuliwaambia tuna uwezo wa kukabiliana nalo ndipo waziri aliposema atatoa tamko,” alisema Mchungaji Makala na kuongeza: SOURCE Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages