KAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI YA TIGO YAKUTANA NA MABLOGGERS KWAAJILI YA KUFAHAMIANA NAO NA KUWEZA KUFANYA NAO KAZI PAMOJA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI YA TIGO YAKUTANA NA MABLOGGERS KWAAJILI YA KUFAHAMIANA NAO NA KUWEZA KUFANYA NAO KAZI PAMOJA

Mtaalamu wa Habari za MItandaoni wa Kampuni ya Simu ya Tigo Bi Samira Bamaar akitoa neno fupi kabla ya hafla iliyowakutanisha bloggers kuanza. Huku pembeni Ni Mmiliki wa Mtandao huu wa Lukaza Blog Mh.Josephat Lukaza (Aliyesimama) akiteta jambo na mmoja wa Bloggers waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika Kebbys Hotel jana
Mmiliki wa Mtandao wa Lukaza Blog, Mh Josephat Lukaza alipokua akijitambulisha wakati wa hafla iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mikononi ya tigo ambao ndio walikua waandaaji wa hafla hiyo iliyowakutanisha mabloggers ili kuweza kufahamiana nao na kuweza kufanya nao kazi pamoja. 
 Meneja wa Huduma za Internet wa Tigo Mh Titus (Aliyenyanyua mikono)Alipokua akitoa maelekezo na ufafanuzi juu ya huduma yao mpya ya Tigo Internet Mega Boksi inavyofanya kazi.
Mtaalamu wa Habari za Mtandaoni wa Tigo Bi Samira Bamaar akifurahi jambo wakati wa hafla fupi tu iliyowakutanisha bloggers, hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Simu ya TIgo
Mmiliki wa Blog ya Kajunason Blog Mh Cathbert Angelo akiwa bize kurusha matukio live kwa muda huo
Baadhi ya Bloggers waliohudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Simu ya Tigo iliyofanyika hotel ya Kebbys hotel jana
Mwendeshaji wa Blog ya Mtaa Kwa Mtaa wa kwanza Kushoto Othman Michuzi akiwa katika Picha ya Pamoja na Mwendeshaji wa Blog ya Missie Popular Mariam na Seif Kabelele
Mmiliki wa Mtandao wa Lukaza Blog, Mh Josephat Lukaza (Wa Kwanza Kulia) akiwa katika Picha ya Pamoja na Mtaalamu wa Habari za Mitandaoni wa Tigo Bi Samira Bamaar (Katikati) na Mwakilishi kutoka Mtandao Wa Mjengwa Blog katika hafla iliyofanyika jana kebbys hotel

Wanamitandao wakiwa kazini kutoka kulia walioshika Camera ni Josephat Lukaza wa Lukaza blog, Zainul Nzige wa Mo Blog na Rajabu Mhamila  Super D wa Burudanblog wakiwajibika katika hafla iliyofanyika Kebbys Hotel jana

Jana Majira ya saa 1 usiku hadi saa nne,blogers mbalimbali walikuwa Kebbys Hotel kwa mwaliko wa Tigo kwa ajili ya kufahamiana na kuona namna wanavyoweza kufanya kazi pamoja.offer kadhaa zimetolewa kwa kupewa line zenye vifurushi vya kutumia bure kwa mwezi mzima.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages