Katibu
Mkuu wa Chadema, Wilbrod Salaa, akiwasili kwenye Ofisi za Makao Makuu
ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, leo mchana kutii amri ya polisi
iliyomtaka kutoa maelezo kuhusu madai yaliyotolewa na chama hicho juzi
kwamba kuna njama zinafanywa na vyombo vya ulinzi na usalama vya
serikali kuwaua baadhi ya viongozi wa chama hicho. Kulia ni aliyekuwa
Mbunge wa Arusha mjini, Godbres Lema.
Askari Poilisi akimuelekeza Dkt. Slaa baada ya kuwasili mahala hapo, ''Haya piteni hapa''.
Baadhi ya watu waliokuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea.
Dkt. Slaa, akiwasalimia baadhi ya watu waliojitokeza mahala hapo.
Baadhi ya wafuasi wa Dkt. Slaa, wakilisukuma gari lake wakati likiondoka mahala hapo, baada ya kuhojiwa. Picha kwa hisani ya Habari Mseto.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)