Balozi
wa Heshima wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon katika jiji la mapesa
la New York City (NYC) nchini Marekani ambaye pia ni mcheza sinema na
mlimbwende maarufu kutoka jiji hilo linaloaminiwa kuwa kitovu cha pesa
duniani, Mmarekani Deidre Lorenz ameahidi kukisadia kituo cha watoto
yatima cha Upendo kilichopo katika Manispaa ya Moshi.
Lorenz
alikitembelea kituo hicho siku mbili (tarehe 22 Juni) kabla ya
kukimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi tarehe 24
juni mwaka huu kuanzia Moshi Club hadi Rau mudukani.
Mbio
za Mt. Kilimanjaro Marathoni zilianzishwa na Marie Frances anayetoka
katika jiji la matajiri la Bethesda nje kidogo ya jiji la Washingyon DC
nchini Marekani mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani nchini
Misri.
Marie
Frances aliyekuwa muandaaji wa vipindi vya television ya ABC
alianzisha mbio za Pyramid Marathon zilizofana sana nchini Misri na
kumfanya balozi wa Tanzania nchini Misri wakati ule kumuomba aje
Tanzania kuanzisha mbio za marathon.
Mt.
Kilimanjaro Marathon ilianzishwa mwaka 1991 katika Manispaa ya Moshi
zikiwa ni mbio kukimbia kwa furaha (fun run) inayowaleta wazungu kupanda
mlima Kilimanjaro, kukimbia na kwenda kutembelea mbuga zetu za
wanyama. Mbio hizi zipo katika kiundi la Seven Continental Marathons
ambazo hukimbiwa katika mabara saba ya dunia.
Deidre
Lorenz ambaye amewahi kuigiza katika filamu nyingi alipatikana katika
bahati nasibu (Raffle) iliyochezeshwa na Mt. Kilimanjaro Marathon 1991
wakati wa mbio za New York Marathon jijini New York Marekani mwaka
2011. Katika bahati nasibu hiyo Deidre Lorenz aliibuka mshindi na
kujipatia tiketi ya bure pamoja na gharama za hoteli za kuja kukimbia
mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon mwaka huu.
Wadhamini
wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon ni kampuni ya ndege ya Ethiopia
Airlines (ET) ambayo huwa inantoa tiketi za bei rahisi kwa wale
wanaokuja kukimbia mbio hizo. ET pia hugharamia ushiriki wa Mt.
Kilimanjaro Marathon 1991 katika mbio za New York Marathon, Boston
Marathon na Los Angelos Marathon ili kijitangaza.
Katika
mpango huo Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 huweka banda la kutangaza
vivutio vya Tanzania kama vile mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama,
Zanzibar na mali zetu za asili.
Mkakati
huu umesaidia sana kuitangaza Tanzania na hivyo kuwapa fursa watalii
wengi kutoka Marekani na nchi nyingi duniani kuijua vyema Tanzania.
Wengi wa wakimbiaji hawa hutembelea vivutio vya Tanzania baada ya
kutembelea banda la Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 katika mbio hizo.
Ufadhili
wa Deidre Lorenz akishirikiana na taasisi ya Screen Actors Guild
utakisaidia sana kituo cha watoto yatima cha Upendo ambacho kinakabiliwa
na changamoto nyingi za fedha na vifaa vya kuwatunza watoto
wanaolelewa kituoni hapo. Kituo hiki kilianzishwa miaka ya 60 na
masista wa shirika la Precious Blood wa Kanisa Katoliki jimbo la Moshi.
Kwa
miaka mingi kituo hiki kimekuwa kinapokea watoto wachanga
wanaotelekezwa na mama zao baada ya kuzaliwa katika hospitali mbalimbali
za mkoa wa Kilimanjaro. Kituo cha Upendo kinawapokea pia watoito ambao
mama zao wamefariki wakati wa kujifungua.
Aidha
Lorenz ameahidi kuwashawishi walimbwende na wacheza filamu wengine wa
Marekani kuja kushiriki katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon na
kutembelea vivutio vya kitalii vya nchi hii kila mwaka.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)