Miss
Sinza 2012, Brigita Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha wakati
akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Judith Sangu (kushoto) na
watatu Esther Mussa, baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo
lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza
Jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Kampuni ya SPM-Sufiani Photo Magic na Mtandao wa
Sufianimafoto.blogspot,com, Nasma Sufiani, akimvisha taji na kumkabidhi
zawadi Maria John, baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumska
Sufianimafoto Miss
Talent, lililofanyika ndano ya shindano hilo la Miss Sinza katika
Ukumbi wa Mawela Social, Sinza jijini Dar es Salaam.
Sufianimafoto Miss Talent, Maria John, akiwa na furaha baada ya kuvishwa taji hilo na kukabidhiwa zawadi yake.
Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) akiwa na
baadhi ya wanakamati wakishuhudia shindano hilo.
Mshiriki, Nancy, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Mshiriki,Naima mohamed, akipita jukwaani na vazi la ufukweni. |
Mshiriki, Maria John, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Msanii
wa Vichekesho, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Uongo Kweli,
akishambulia jukwaa, wakati wa onyesho hilo na kuwapagawisha vilivyo,
mashabiki wa fani ya urembo waliokuwapo ukumbini hapo.
Mshiriki, Mariam Miraji, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia shindano hilo.
Madj
wa Sufianimafo, wakiwa katika mitambo ya Sufianimafoto, iliyokuwa
ikitumika katika shindano hilo, wakiendesha shughuli nzima ukumbini
hapo.
Pozi
la Masawe Mtata, kabla hajapanda jukwaani, huku akiwa ameketi na
wanadada ambao baada ya kushuka jukwaani walianza kumgombea, ''he kumbe
tumekaa na Masawe hapa hatujui, hebu nipe namba yako'', wasilikika
madada hao wakisema kila mmoja akiomba namba huku mwingine akisikika
kumpiga mkwara Masawe, ''Ole wako umpe namba huyo mdada ntakupasua''
alsema mdada mmoja kati ya hawa walionyuma yake kana kwamba yeye alikuwa
tayari amekwisha wini kupata namba.Picha na www.sufianimafoto.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)