Meneja
Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya “Daka Salio”
iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel , pichani kushoto ni Afisa
uhusiano wa Airtel na kulia ni Meneja bidhaa wa Airtel Salim Madati
Afisa
mawasiliano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akifafanua kuhusu
huduma ya mpya ya “Daka Salio” wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo
uliofanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Moroco na kuhudhuria
na waandishi wa habari, katika ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando akifatiwa na Meneja Bidhaa Salim Madati
Maafisa
wa Airtel kwa pamoja wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya “Daka
Salio” wakati wa uzinduzi Uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika katika
makao makuu ya ofisi za Airtel Moroco na kuhudhuria na waandishi wa
habari, kutoka kushoto ni Afisa mawasiliano na matukio Bi Dangio Kaniki,
Meneja Uhusiano Jackson Mmbando na Meneja Bidhaa Salim Madati
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuendeleza dhamira yao ya Uhuru wa
kuongea imetoa fulsa nyingine kwa wateja wake kwa kuzindua huduma
kabambe ya Daka salio ikiwa ni jitihada zake katika kutimiza dhamira
yake ya kuendelea kutoa uhuru wa kuongea kwa wateja wake nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando by
Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kuleta huduma hii ya Daka salio kwa
wateja wetu wote waendelee kufurahia huduma zetu kila wakati, ikiwa
sasa unaweza kukopa na kuongea na ndugu au rafiki wa mtandao wowote sasa
hakunakubeep tena.
Hii
ni huduma nzuri kwa familia, marafiki ndugu au jamaa kwa kuwa itaondoa
tatizo la watu kubeep, Airtel tunasema kwanini ubeep au uteseke kukopa
kiwango kikubwa na kulipa zaidi. Daka salio kidogo na ulipie kidogo na
airtel. Ili kufurahia huduma hii ni rahisi na haraka tuma tu neno daka
kwenda 15549. Uongee mwanzo mwisho, kwa raha zako.
Mteja
yeyote anaweza kukopa ikiwa tu amekuwa mteja wa Airtel kwa
mfululizosiku tisini, awe anasalio la hadi shilingi 50 na asiwe anadaiwa
deni la Daka salio ikiwa alishakopa kupitia huduma hii.
Faida
ya kukopa salio ya Airtel ni kwamba tunakukopesha kiwango kidogo
ambacho utalipia kiduchu tu na utaongea kwa muda mrefu. Achana na
wanaokopesha kiwango kikubwa halafu unaongea kidogo.
Mteja
wa Airtel anaekopa salio kwa daka salio ataweza kukopa sh 180 na
akitaka kulipa atalipa ziada ya sh 18 tu yaani atatoa jumla ya 198 tu,
kwa hiyo hata ukiongeza salio la sh 500 bado utabakia na salio la
kukuwezesha kufurahia uhuru wa kuongea toka Airtel.
Airtel
imekuwa na ubunifu wa bidhaa na huduma zake zaidi kwa lengo la
kufaidisha jamii kwa ujumla. Hivi karibuni ilizindua huduma ya SUPA 5
yenye dili tano bomba na inaendelea kutoa unafuu kwa wateja wa Airtel
kupata sms 200 bure, kuongea na watu watatu kwa nusu shilingi siku
nzima, kupata huduma ya facebook bure , intaneti bure usiku, pamoja na
kongea kwa robo shilingi nyakati za usiku kwa kupiga tu*149*99# na kufuata utaratibu.
Airtel
pia kupitia huduma yake ya Airtel money inawawezesha wajasiliamali
waliowekeza katika kwa kuwa wakala wake nchi nzima pamoja na wateja
wake, kwa wateja sasa wanapata mara mbili ya salio wanaloongeza
kupitia huduma ya Airtel Moneywakati WAKALA wote nchi nzima watapata
mara mbili ya kamisheni zao kwa mwezi juni - julai kwa mihamala yote
watakayofanya kupitia Airtel Money.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)