Akizungumza katika mahojiano na Redio One, Msajili huyo wa vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, alisema kuwa anatambua uwepo wa vyama vingi vya Siasa, lakini baadhi yao vimekuwa kimya zaidi ambapo huanza kuibuka wakati wa Kampeni na uchaguzi Mkuu.
Alisema kuwa hivi sasa wapo katika mchakato wa kuvifuatilia vyama vyote ambavyo haviwajibiki kwa jamii na kusubiri kujitokeza wakati wa uchaguzi na kusema kuwa endepo vitakavyogundulika vitafutiwa usajili.
Miongoni mwa vyama vitakavyokumbwa na kimbunga hicho ni vile visivyokuwa na uwakilishi wa wananchi katika nganzi mbalimbali za Udiwani, Uenyekiti na Ubunge.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)