MWENGE WA UHURU WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM, MIRADI YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 7 KUZINDULIWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWENGE WA UHURU WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM, MIRADI YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 7 KUZINDULIWA

Mkuu wa mkoa wa Dar es  Salam Saidi Meck Sadik (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Tatu Saidi Mussa leo jijini Dar es Salaam . Mwenge wa Uhuru umewasili  jijini  Dar es Salaam ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akiahidi mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadik kuupokea Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo miradi 11 itafunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo.
Askari kutoka jeshi la Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa sherehe za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
Wakimbiza Mwenge kitaifa wakiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Capt. Ernest Mwanossa (wa kwanza mbele)  wakianza safari kuelekea maeneo mbalimbali ya wilaya ya Temeke leo jijini Dar es Salaam.
Vijana wa halaiki kutoka wilaya ya Temeke wakiimba wimbo maalum wa Mwenge wakati wa mapokezi leo jijini Dar es Salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages