Simu yasababisha gari kuteketea kwa moto! - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Simu yasababisha gari kuteketea kwa moto!

FULLSHANGWEBLOG inashuhudia muda huu Moto unaoteketeza gari aina ya Mercedes Benz ML Class ambalo namba zake hazikupatikana mara moja baada ya moto kuwa mkubwa, Gari hilo lilipoteza mwelekeo na kuingia mtaroni na kushika moto. Ajali hiyo imetokea mchana huu katika barabara ya Kilwa eneo la Tanesco, Mivinjeni. Mmoja wa mashuhuda ambaye alikuwa na gari lingine nyuma ya gari hilo kabla ya ajali, amesema dereva wa gari hilo alikuwa akiongea na simu kabla ya ajali hiyo! TAHADHALI: USITUMIE SIMU UKIWA UNAENDESHA!.Picha Kwa Hisani Ya Full Shangwe Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages