Meneja
Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson
Mmbando akimkabidhi Jamila Juma simu ya mkononi aina ya Sumsung,baada
kuibuka mshindi kwa kuichammbua vyema huduma mpya ya Airtel Jiunge na
Supa5.
Pichani
shoto wakazi wa Mwanza, Jamila Juma na Sandra Mwashitete wakipewa
maelekezo mafupi namna ya kutumia mtandao wa Airtel pamoja na huduma
zake mbalimbali, mara baada ya kujishindia simu aina ya Sumsung,wakati
kampuni ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge
na Supa5,uliofanyika jana kwenye viwanja vya Furahisha,jijini Mwanza.
Ni
Mzee wa Makamo hivi lakini alionesha umahiri wake mkubwa wa
kuwachangamsha vilivyo sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza.Anaitwa Mzee
Salum akikamua jukwaani jana kwenye viwanja vya Furahisha jijini
Mwanza,wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
Sehemu
ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jana jioni kwenye
uzinduzi ramsi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika
kwenye viwanja vya Furahisha jijini humo.
Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya na kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi
kutoka Temeke,jijini Dar,akiwa sambamba na msanii mwenzake (hayupo
pichani) aitwaye Kr-Mulla wakilishambulia jukwa huku shangwe kubwa
ikilipuka kutoka kwa sehemu kubwa ya wakazi wa jiji la Mwanza
waliojitokeza jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel
Jiunge na Supa5.
Baadhi
ya wasanii wa kikundi cha Kinonko chenye maskani yake pale
Kinondoni,kikionesha umahiri wake wa kucheza mbele ya umati mkubwa wa
wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye viwanja vya Furahisha
wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
.Baadhi
ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakiendelea kuhamia Airtel na kupata huduma
mbalimbali za kampuni hiyo,jana jioni kwenye viwanja vya Furahisha
wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)