Viongozi mbalimbali kutoka ubalozi wa China na seraikali ya Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza hafla fupi ya kusherehekea mafanikio
ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye
miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania.Kutoka kushoto nyuma ni
balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule.
Baadhi ya mashuhuda wa miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ukiwemo ujenzi wa reli ya Uhuru (TAZARA) walioalikwa kwenye hafla hiyo Bw.
Abdul Haji (kulia) na mama Roza Kangoma (kulia) ambaye ni mama wa
balozi wa Zambia nchini Tanzania pia aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha
mafunzo cha TAZARA.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia)
akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa na ubalozi wa China nchini
Tanzania kuhusu mikakati ya serikali ya kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao wakati wa hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayofanyika Tanzania.
Wageni
mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo katika ubalozi wa China nchini
Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
Raia kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kusherehekea mafanikio
ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kutoka nchini China katika miradi
mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania wakijipatia nakala mbalimbali za
machapisho kuhusu shughuli za kilimo, siasa, Utamaduni, Teknolojia na
masuala ya kijamii.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)