Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Leph Gembe akiingia Ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) aliyemaliza muda wake Bw Emmanuel Misungwi katika ukumbi wa veta uliopo Mkoani Dodoma katika Sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu Mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini (Wa Pili Kushoto) Mh Leph Gembe akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) ambao wamemaliza muda wao ambapo wa kwanza kushoto ni Mwalimu mlezi wa taasisi hiyo Bw. Jeremiah katika sherehe ya Kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao wanasoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiingia ukumbi kwa staili ya kucheza kwaito katika sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu iliyofanyika katika ukumbi wa veta uliopo dodoma mjini
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu iliyofanyika katika ukumbi wa veta uliopo mjini Dodoma
Mwenyekiti Wa Kwanza na Muasisi wa taasisi hii ya wanafunzi wanaosoma sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ambaye amehitimu mwaka 2011 Mh Ibrahim Bakari akitoa neno wakati wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa veta
Makamu Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bi Gaundensia Mwakemwa akimvalisha kitambulisho Makamu Mwenyekiti Mpya Bw Mtono Juma kama ishara ya kukabidhi madaraka kwa viongozi wapya wa taasisi hiyo.
Mwenyekiti mpya wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma Bw Edgar Kelvin akimkabidhi zawadi mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Leph Gembe ambaye pia alikua mgeni rasmi wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma
Wadada safi kabisa wakiwa wamebeba keki tayari kwaajili ya kuikata
Wawakilishi wa wanafunzi walioitwa mbele kwaajili ya kukata keki kutoka kushoto ni Mwanafunzi Loyce Haule, Katikati ni Shabani Kambi na Mwisho kabisa Ni Beatrice Msami
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tatu na viongozi waliomaliza muda wao wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu Mpya Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Leph Gembe kama ishara ya kutambua majukumu yao kipindi wakiwa katika nafasi za uongozi
Muda wa Maakuli huo
MWENYEKITI WA KWANZA NA MUASISI WA UNIVERSITY OF DODOMA SOCIOLOGY
STUDENTS ORGANIZATION(UDOMSSO) AMBAYE AMEHITIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA
DODOMA (UDOM) MWAKA 2011 NDUGU IBRAHIM BAKARI (Wa kwanza Kushoto)
KATIKA PICHA YA PAMOJA NA AFISA HABARI WA UDOMSSO ALIYEMALIZA MUDA WAKE
JANA NDUGU JOSEPHAT LUKAZA KATIKA SHEREHE YA KUTUAGA MWAKA WA TATU
TUNAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA
Raha ya Sherehe ni kula, kunywa na kilichobaki ni kucheza wadau wakiserebuka mduara
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)